Sunday, July 19, 2015

Adui mpole.

No comments


Teknolojia imechukua nafasi kubwa katika maisha yetu ya kika siku. Kuanzia simu za kiganjani, magari, gari moshi za mwendo kasi, ndege za abiria zitumiazo nishati mbadala ya jua na mengine mengi. 
Watu wengi wamekuwa wakifurahia teknolojia hizi na kuzitumia mara kwa mara bila kujua athari na madhara yake. Fahamu athari za teknolojia katika nyanja mbalimbali:- 

1. Familia 
Teknolojia imechangia kwa kiasi kikubwa Kuvunjika kwa ndoa pamoja na watoto kukosa maadili. 
Mitandao ya kijamii imehusishwa kwa kiasi kikubwa katika kuanzisha mahusiano yasiyo rasmi kati ya mwanandoa mmoja na mtu mwingine, kitu kinachofanya ndoa nyingi kuvunjika. 
Pia mambo mengi yasiyo na maadili huwekwa katika mitandao, ambapo vijana wengi hupenda kuyaiga na kuwafanya wao wakose maadili. 

2.Afya 
Magonjwa kama cancer na upungufu wa nguvu za kiume yanawapata watu wengi kwa sasa kutokana na teknolojia tunazotumia kila siku. Matumizi mabaya ya teknolojia hizi huharibu mifumo mbalimbali katia mwili wa binadamu. 
Wataalamu na madaktari wamekuwa wakishauri matumizi sahihi ya simu, laptop, x-rays na vifaa vingine. 
Mfano: watumiaji wa laptop wanashauriwa kutoweka laptop hizo mapajani kwa mda mrefu kwani kunaweza wasababishia ugonjwa wa cancer. 

3. Elimu
Licha ya kuwepo kwa teknolojia nyingi zinazo rahisisha upatikanaji wa elimu, bado kumekuwepo na matumizi mabovu ya teknolojia yanayo zorotesha maendeleo ya elimu. 
Mfano: watoto kupoteza mda mwingi katika michezo ya tv (video games), mitandao ya kijamii, na hata filamu, mambo haya yanawakosesha mda wa kurejea masomo ya darasani. 

4.Uharifu
Teknolojia inahusishwa katika uharifu unaotokea sasa kwa kiasi kikubwa. Mtu anaweza akawa Marekani lakini akaiba pesa katika benki iliyopo Tanzania kwa kutumia teknolokia ya mtandao. 

Haya ni baadhi ya madhara na athari zinazosababishwa na matumizi ya kila siku ya teknolojia. Ni vyema kujua matumizi sahihi ya teknolojia tunazozimiliki ili kujikinga na athari na madhara yake. Pia ya yatupasa kufuata ushauri wa Wataalamu na madaktari kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia.