Kumekuwa na vikwazo vingi vinavyosababisha wanafunzi kushindwa kufanya majaribio ya kutosha ya masomo wanayosoma.
Vikwazo hivyo ni pamoja na mda mdogo mashuleni, wazazi kushindwa kuyamudu masomo wanayosoma watoto wao na kadharika.
NIPIME ni programu tumishi inayowezesha wanafunzi wa sekondari kufanya majaribio ya hesabu na fizikia kwa kutumia simu zenye mfumo wa android. Mtumiaji wa nipime hufanya jaribio moja lenye maswali matano kisha majibu yake huhakikiwa kama ni ya sahihi au siyo.
Baadae, programu hiyo huonesha alama (maksi) alizopata mtumiaji huyo kulingana na maswali aliyojibu sahihi.
Mtumiaji haitaji kuwa na mtandao wa internet ili kutumia programu hii, jambo linaloifanya programu hii kuwa ya pekee kwa kujali uchumi wa wanafunzi na wazazi pia.
Pia programu hii inaonesha ni kwa kiasi gani teknolojia inaweza leta mabadiliko katika nyanja ya elimu Tanzania, kwani sasa mzazi yeyote bila kujali kiwango chake cha elimu anaweza mpa mwanae majaribio mbalimbali na kuyafanya.
Programu hii inapatikana Play store kwa jina la nipime, BOFYA HAPA kuipakua Au kupitia tovuti maalumu kwaajili ya programu hii: nipime.edumek.com
"soma popote, mda wowote ukiwa na mtu yoyote "