Wednesday, August 03, 2016

Hatimaye China yakamilisha utengenezaji wa basi kubwa linaloweza pita juu ya magari mengine.

No comments

Transit Elevated Bus (TEB)

Wengi tulishuhudia video zikitawala mitandao ya kijamii kwamba kuna basi kubwa linaloweza beba watu wengi (abiria 300 kwa makadirio)lakini pia linaweza ruhusu magari mengine kupita chini yake, nasi sote tukazani ni uwongo au ni wazo ambalo halitaendelezwa.
Hatimaye nchi ya china imeweka historia  baada ya kukamilisha Utengenezaje wa usafiri huo ambao utaanza jaribiwa na kutumika hivi karibuni.

Basi hilo lililopewa jina la Transit Elevated Bus (TEB), linauwezo wa kubeba abiria 300 ,lina upana wa futi 25 na urefu wa futi 72. Pia basi hilo lina speed inayofikia 64Km kwa saa.


Baada ya china kutengeneza basi hili nchi kama Brazil, France, India na Indonesia zimeonesha nia ya kuwa na usafiri kama huo.
Kwa jinsi jiji la dar es salaam lilivyo na foleni, usafiri huu ungefaa sana.


Jionee video inayoelezea zaidi kuhusu usafiri huo.



kuona video nyingi zaidi za uzinduzi wa basi hilo ingia hapa:: zhongguowangshi.com

Imeandaliwa na @blessmgongolwa