Tuesday, June 02, 2015

Fahamu Njia 10 zitakazo kuwezesha kuwa salama unapotumia mtandao wa internet

No comments

Watu wengi wamepata matatizo kwa sababu ya matumizi yasiyo salama ya mtandao wa Internet, kuanzia malicious software, wizi wa kimtandao,virus na hata uharifu mwingine wa kimdandao.
Zifahamu njia kumi zitakazo kuwezesha wewe na kifaa chako kuwa salama pindi unapotumia Internet.

1. Usitumie password moja sehemu zote.
 - Usipende kutumia password ya aina moja katika mitandao na huduma zote, kwa njia hii waharifu wataweza kuvamia mitandao yako yote pindi watakapoijua password yako.
Mfano. Sio salama kutumia password moja kwenye facebook na twitter.

2. Epuka mafaili ya torrent.
 - Imezuka tabia ya watu wengi kupenda kudownload vitu mbalimbali kwa kutumia torrent. Njia hii ni hatari kwani waweza download faili lilojumuisha software ambazo zitaharibu utendaji kazi wa computer yako.

3. Kuwa mwangalifu na viambatanisho vya email (email attachments).
- Usipende kufungua mafaili yaliyoambatanishwa kwenye email bila kujua usalama wa mafaili hayo, ni vyema kuweka software au app itakayoyaangalia kama mafaili hayo ni salama.

4. Linda taarifa zako muhimu.
- Ni vyema kulinda taarifa zako muhimu kabla ya kutumia internet. Taarifa kama namba ya siri ya kadi ya benki na password za mitandao mingine ziko salama na haziwezi kufikiwa na wahalifu.

5. Siku zote penda kuinstall updates.
- penda kuinstall updates za software, apps au os ya kifaa pale inapofika wakati wake. Kazi muhimu ya updates hizi huwa ni kupunguza mapungufu ya software au kifaa hicho na kukifanya kiwebora zaidi.

6. Usipende kufungua links kwenye email usizo husika nazo.
- Wezi wa kimitandao hutumia njia nyingi ikiwemo hii ya kutuma link kwa njia ya email. Hivyo usipende kufungua link kutoka email usiyo ifahamu.

7. Siku zote nunua vitu kwanjia ya mtandao kupitia HTTPS.


- hakikisha mihamala yote unayofanya kwa njia ya mtandao inapitia katika njia salama ya HTTPS. Website zenye huduma hii utaona link zake zikiwa zinaanza na neno HTTPS na maneno hayo huwa yana rangi ya kijani.

8. Boresha mifumo ya ulinzi na usalama ya kifaa chako.
- Boresha mifumo ya muhimu ya ulinzi yakifaa chako ili kuwa na uhakika kuwa uko salama.

9. Wazuie watu wengine kutumia kifaa chako pale inapobidi.
- Kama kifaa chako kina taarifa muhimu ambazo usingependa watu wengine kuziona ni vyema kuzuia watu kutotumia kifaa hicho pale inapobidi.

10. Kuwa makini na mitandao ya bure ya wiFi (public wifi). - Mara nyingi ni rahisi kwa Wezi wa mitandao kukamata data zinazotumwa kwa njia ya mtandao kwa watumiaji wa wifi. Hivyo jihadhari na matumizi ya wifi.

Njia hizi zitakusaidia vya kutosha katika kuhakikisha uko salama pamoja na kifaa chako.