Showing posts with label afya. Show all posts
Showing posts with label afya. Show all posts

Tuesday, September 01, 2015

UTAFITI: Kulala mchana kunazuia mshutuko wa moyo

No comments

Uchunguzi unaonyesha kuwa kulala wakati wa mchana kunapunguza shinikizo la damu na pia kupunguza hatari ya kupatwa na mshutuko wa moyo pamoja na kiharusi.

Kulingana na utafiti, kulala kwa muda wa nusu saa ua zaidi wakati wa mchana hupunguza hatari ya kupatwa na mshutuko wa moyo kwa hadi asilimia 10.

Takriban watu 400 waliokuwa na shinikizo la damu walishiriki katika utafiti uliofanywa nchini Ugiriki. Matokeo ya utafiti huo yaliwasilishwa katika chama kinachohusika na masuala ya damu barani ulaya.

Watafiti sasa wanataka kufanya uchunguzi zaidi kuhusu matokeo yanayotakana na watu kulala saa za mchana.

Chanzo: BBC Swahili

read more

Wednesday, August 05, 2015

Je unataka kuishi maisha marefu duniani ?

No comments

Utafiti mmoja uliofanywa nchini China umebaini kuwa ukila chakula kilichotiwa viungo kila siku unajiongezea maisha marefu.

Utafiti huo haswa umeonesha kuwa ukila chakula hususan pilipili utaishi maisha marefu zaidi duniani.

Watafiti mjini Baijing walidadisi maisha na vyakula wanavyokula wenyeji nusu milioni katika kipindi cha utafiti cha miaka 7.

Utafiti huo ulibaini kuwa wale waliokula chakula kilichojumuisha pilipili walikuwa katika hali bora zaidi kiafya wala hawakuwa katika hatari ya kuaga dunia.

Hali yao ya siha ilitofautiana sana ikilinganishwa na wale ambao waliweka viungo katika vyakula vyao chini ya siku moja kwa juma .

Watafiti hao walitoa tahadhari.

Wanasema kuwa utafiti huo ulikuwa wa ushahidi tu lakini wakashauri utafiti zaidi ufanyika kwengineko ilikutilia pondo utafiti wao.

Hata hivyo walibaini kwa uhakika kuwa kiungo kinachopatikana katika pilipili, 'capsaicin' kinauwezo wa kupigana na seli zinazotuma ujumbe kwa ubongo kuwa mtu amezeeka na kusababisha viashiria vya utu uzima.

CHANZO: BBC Swahili

read more