Showing posts with label Uchaguzi2015. Show all posts
Showing posts with label Uchaguzi2015. Show all posts

Monday, October 26, 2015

Julius S. Mtatiro: HATUWEZI KUSHINDA UBUNGE SEGEREA

No comments

Ujumbe uliopatikana kutoka katika ukurasa wa facebook unaoaminika kumilikiwa na Julius s matatiro umeeleza kwanini hawataweza kushinda Ubunge katika jimbo la Segerea.

" HATUWEZI KUSHINDA UBUNGE SEGEREA...

Ndugu zangu, kwa moyo mkunjufu kabisa napenda kuwajulisha kuwa hatuwezi tena kushinda ubunge wa jimbo hili kwenye uchaguzi uliofanyika jana.

Matokeo ya majumuisho ya kila kata yanaonesha kuwa mgombea wa Chadema, Bi. Anatropia Theonest ana wastani wa kura 2000 - 2500 kwa kila kata.

Mimi nina wastani wa kura 4000 - 5000 kwa kata na mgombea wa CCM ana wastani wa kura 5000 hadi 6000 kwa kata.

Hii ina maana kuwa kura za UKAWA kama zingelipigwa kwa mgombea halisi wa UKAWA tungeishinda CCM kwa zaidi ya kura 20,000 lakini kwa sababu zimepigwa kwenda vyama viwili tunaweza kushindwa kwa wastani wa kura 5000 hadi 10,000.

Haya yaliyotokea hapa Segerea ni funzo kubwa kwa vyama vyetu na wanasiasa wetu kuheshimu na kusimamia makubaliano, kuwa na roho ya kufikiria mustakabali wa taasisi na watu wetu kuliko MASLAHI BINAFSI. Kwa hatua ya sasa sitaeleza hujuma za ndani kwa ndani tulizofanyiana ndani ya UKAWA hadi kufika hapa.

Nachoweza kusema ni Asante Mungu na asante wana Segerea, asante watu wote waliojitoa kufa na kupona kutusaidia, lakini pia asante kwa wale wote waliotusaliti kimya kimya ili kuchochea mgawanyiko wa kura hizi.

Naahidi kushiriki katika hatua zote za kumsaidia mshindi wa uchaguzi wetu ili atangazwe rasmi kuwa mbunge wa wana Segerea. Mimi nitaendelea na majukumu mengine lukuki ya kulijenga taifa letu.

Kwa sababu yaliyosababisha kukosa ushindi wetu ni mambo ya ndani ya vyama vyetu, sitachukua hatua zozote wala kukata rufaa kwa sababu wananchi hawakutunyima ushindi, tumeugawanya wenyewe.

Nawapongeza madiwani wa UKAWA walioshinda kwenye kata zote 13 za jimbo letu, tulishirikiana na kupambana pamoja hadi kuleta ushindi huu, nawataka wachape kazi kufa na kupona na waisimamie manispaa ya Ilala bila woga, nawaomba wakatumie mipango na ushauri tuliowahi kupanga pamoja ili kuwatendea wana Segerea yale waliyoyatarajia.

Mwisho, nataka kuwaeleza watanzania wote kuwa sina kinyongo na mtu yeyote kwa matokeo haya. Mimi ni kati ya watu wanaoamini kuwa SIASA SI AJIRA...Nitaendelea kuwatumikia watanzania kwa njia zote muhimu nje ya vyombo vya maamuzi.

Nataka kuwaambia wananchi wa Segerea kwamba niko imara sana, sijayumba wala kutetereka, nawapenda sana nyote na poleni na MSHTUKO wa matokeo haya na muda si mrefu tutayaweka hapa.

Ni mimi,
Mtatiro Julius,
Segerea.
"

Chanzo: ukurasa wa facebook

read more

Matokeo Mengine ya awali kwa wagombea Urais wa jamuhuri ya Mungano wa Tanzania

No comments

Majimbo ya Lulindi, Paje, Makunduchi, Donge, Mkoani, Chambani na Kiwani.

read more

Matokeo ya awali kwa Jimbo la Bumbuli na Kibaha Mjini

No comments
read more

Sunday, October 25, 2015

Taarifa Rasmi Kutoka UKAWA Kuhusu Uchaguzi Mkuu Unaoendelea Leo- 25/10/2015

No comments

1. Hali ya vitisho vya jeshi la polisi na kamata kamata iliyoanza jana usiku hadi leo asubuhi. Wawaache wananchi watumie haki yao ya kikatiba kumchagua kiongozi wanayemtaka. 

2. Suala la watu wenye kadi lakini majina yao hayapo, ambapo kisheria inatakiwa msimamizi awape fomu namba 19 kisha waijaze na kupiga kura. Tumewataka wananchi kutokuondoka vituoni hadi wapate haki hiyo ya kujaza fomu hizo na kupiga kura. 

Vifaa vya kupigia kura kuchelewa kufika vituoni ambapo baadhi ya vituo kama Kimara Temboni Dar es salaam, msimamizi amefungua kituo saa mbili kisha akasema karatasi za mgombea urais zimekwisha. Tumewataka wananchi katika maeneo kama hayo kutokuondoka vituoni, wakae kwa utulivu wahakikishe wanapiga kura.

Tumewataka NEC ambao wanapigiwa simu lakini hawapokei kutoa msaada wa haraka, wahakikishe suala hilo linatatuliwa haraka. Uchaguzi huu haukuwa ajali au suala la kushtukiza. 

3. Idadi ya wapiga kura kwenye kituo kimoja kuwa kubwa tofauti na matakwa ya kisheria, kuna vituo tumebaini vinawapiga kura zaidi ya 800. Hairuhusiwi. Wapiga kura hawapaswi kuzidi 450 kwa kila kituo.

4. Madai ya kuwepo kwa kura feki kukamatwa katika maeneo mbalimbali zikiwa tayari zimepigwa, mfano tunazo taarifa za kukamatwa huko, Vunjo, Njombe na maeneo mengine ya nchi. 

Hili tulitarajia tume ilizungumzie kwa udharura lakini mpaka sasa tunawatafuta watu wa tume hawapatikani. 
Tunawahimiza watu wawe watulivu wasiondoke vituoni mpaka wapige kura ambayo ni haki yao kikatiba. 

Tumaini Makene 
Mkuu wa idara ya mawasiliano 
CHADEMA

Chanzo: chadema blog

read more

Wednesday, October 21, 2015

Jonathan advises Tanzanians on need for peaceful polls

No comments


Former president, Dr. Goodluck Jonathan yesterday advised the Tanzanian National Electoral Commission, political parties and civil societies to ensure peaceful and transparent electoral process. Jonathan gave the advice on arrival as the chairperson of the Commonwealth Observer Group (COG) to Tanzania’s October 25 general elections. Jonathan said only a credible voting process would confer legitimacy on a democratic government. A statement quoted the former president in Dar Es Salaam as saying that the success of the polls would depend on every stakeholder. “During our time in Tanzania, we will seek to assess the pre-election environment, polling day activities and the post-election period, against the backdrop of Tanzania’s national legislation, regional and international commitments. “We will perform our observation role with impartiality, independence and transparency. On Friday, October 23, on election day, they will observe opening, voting, closing, counting and the results management process and issue an interim statement on our preliminary findings shortly after the elections. A final report will be prepared in Tanzania. It will be submitted to the Secretary-General, and subsequently shared with relevant stakeholders and the public. The group is scheduled to depart Tanzania on October 31.”
read more

Tuesday, October 20, 2015

January Makamba: 10 reasons why Tanzania’s ruling party will retain power in Sunday's election

No comments

THIS month, Tanzanians go to the polls in what must be seen as the most eventful election since the reintroduction of multi-party democracy in 1995. There’s been great interest in this contest in a country of over 50 million, in part because some commentators believe that this time, the opposition has a chance to unseat one of Africa’s largest and best-organised political parties, the governing Chama Cha Mapinduzi (CCM) or “Party of the Revolution”. Certainly, this is a riveting story: but it is just that - a story.

I have the benefit of being part of the CCM campaign team. Through relentless voter research and, for the first time, the use of internationally acclaimed campaign techniques, it’s possible to see things differently. Here are 10 reasons why we are certain John Pombe Magufuli, the CCM candidate, will be elected the next president of the United Republic of Tanzania.

1.   Edward Lowassa’s flawed candidacy

Having won every multi-party poll since the mid-1990s, the simple passage of time suggests that this was going to be tough election for CCM irrespective of who was the opposition’s presidential candidate. But the election was tilted in CCM’s favour the day the opposition anointed former Prime Minister Edward Lowassa as their candidate in August, without any internal vote.

Proclaimed as popular and one of those most tipped to win the CCM nomination for President before he was defeated in the party’s internal election, this is as counterintuitive as it is true.


It is easier for CCM to win against Lowassa than it would have been against Wilbrod Slaa, presidential flagbearer of the opposition at the last election, and likely candidate this time before he was pushed aside to make room for Lowassa. Slaa is universally respected for his honesty and oratory, and, because of this, occupies a moral high ground on many issues with credibility. Lowassa cannot take on this mantle. He is now running against the very establishment he helped create and was married to all his life until only two months ago.

The CCM did not elect Lowassa as its presidential candidate because he could never be a candidate of change, because of his history. Indeed, had he stood for CCM he would personify everything voters have told us is wrong with a party that has long been in government.  There are those who believe that this is a tough election for CCM because Lowassa is the opposition nominee. We believe it could have been far tougher for us had he been our candidate.

2.   The opposition has ceded the anti-corruption agenda

The past 10 years have been eventful as far as the exposure and prosecution of corruption; media, civil society and parliament have pushed this agenda in response to public discourse. Outgoing president Jakaya Kikwete made history by ordering the government’s Controller and Auditor General’s reports publicly available and debated in the parliament. Yet during this same period Lowassa was forced to resign as prime minister because of a corruption scandal. It is clear the public has been awakened to the fact corruption, even at the very top, is not acceptable, and that there are consequences for those who indulge in it.

It means that Lowassa creates an insurmountable challenge for an opposition that, until his coronation, had made its name fighting corruption. Indeed, US Embassy cables exposed by Wikileaks went to the length of stating “Lowassa’s corrupt activities have been an open secret throughout Tanzania for many years”, egregious as they had become. The fact is such allegations were so publicly known that in 2007, at the height of opposition rallies against corruption, they publicised a “List of Shame”, with Lowassa topping the list.

So, far from this election becoming an opposition-led referendum on corruption – as it might have been had Lowassa been the CCM candidate – it has become a referendum on the past corruption of Lowassa and his suitability for public office. Once Lowassa was chosen as the opposition candidate, Slaa and Prof. Ibrahim Lipumba - key opposition figures since 1990s - resigned from leadership positions in disgust.

As a result, this is an election campaign in which the opposition tore up their trump card – a powerful narrative against corruption. So far has opinion travelled on this subject, they are now on the defensive. One opposition Member of Parliament, Peter Msigwa, in a TV debate, went so far as to say that, in courting Lowassa, the opposition had conducted research and discovered that “corruption is not an issue in this country”. Yet through once promoting their List of Shame the opposition had claimed publically they had such evidence. This is clearly very different voter research than that which we have conducted amongst 20,000 voters in the last month.

This is a crucial election for the opposition. Indeed, it has existential implications. Failure to make a credible showing in October may condemn them to also-rans for another decade. That is why it beggars belief that they have chosen to run away from the one issue that has so defined and elevated their cause, and that so energises and resonates with voters.

3.   Change you can’t believe in

Reading the words the opposition posters across the Tanzanian capital Dar-es-Salaam decrying “It’s time for change” is a very different experience from seeing the two main headliners at opposition rallies - former prime ministers Frederick Sumaye and Lowassa. Jointly, before August, they had been in CCM and in senior government positions for over 50 years. It is beyond comprehension for many voters to hear them rail against the establishment that they built, that shaped their political behaviour and that they were praising only two months ago.


To hear them claim the CCM has done nothing when they were leading members of the government for an entire generation is to hear them condemn their own leadership. A Damascene conversion to the opposition only two months ago cannot undo decades of history. Neither in form, nor style nor substance, can they represent change.

4. Conflict and confusion in the main opposition alliance (UKAWA)

In each of the last two election cycles the opposition has attempted to unify to unseat CCM, and each time, the unity crumbled. In advance of this election, last year they settled on a new common policy that might unite a group of regional parties – a draft constitution calling for 3-tier government. Then they chose to translate that unifying objective into an electoral unity through fielding a single presidential candidate and apportioned constituencies to each party in the coalition.

Then came the undoing: despite their umbrella coalition “UKAWA” having ‘democracy’ and ‘development’ in its name – they reneged on their formula of electing a single presidential candidate, and instead anointed Lowassa. Their belief was that Lowassa’s entry into UKAWA would prompt the leading figures in the CCM to also defect. Instead it caused the resignation of two prominent opposition leaders –Lipumba and Slaa. Other prominent opposition members of parliament have deserted to ACT-Wazalendo, a new opposition party that stayed out of the broad opposition coalition.

Now UKAWA’s plans to field one parliamentary candidate for each constituency has crumbled. In one constituency, Masasi, Lowassa’s man had to be rescued from the stage as the crowd chanted that they would now vote CCM. In another constituency, Nzega, Lowassa had to call a voice vote where the crowd was asked who they would prefer between the two opposition candidates. Because of this chaos CCM is in play to win parliamentary seats against a divided opposition in the assembly elections also on General Election day that may otherwise have been out of their reach.

5. Lowassa’s helicopter campaigning

Lowassa has chosen to campaign by helicopter, holding large rallies in regional capitals, followed by a few local constituency visits. He then returns to Dar-es-Salaam. The reasoning behind this is uncertain, but it does not demonstrate a desire to truly meet voters face-to-face. Contrast this with the CCM candidate Magufuli who travels by car, reaching village after village, holding eight to twelve rallies each day. This kind of interpersonal campaign is in keeping with Tanzania’s style: informal and open, and reaches into rural areas when the media from cities and towns does not.

It’s undeniable that Lowassa generates big crowds in the major cities. But the record for numbers at a rally is still held by Augustine Lyatonga Mrema, the opposition candidate in 1995 (who had also defected from CCM) who lost that election by over 30 percentage points.

6. All politics is local

In Tanzania, few organisations can rival CCM’s ability to mobilise citizens. While the opposition is seduced by the romance of the campaign, big rallies and newspaper headlines, CCM deploys its organisational prowess on the ground. Structurally and organisationally, CCM’s Women Wing alone has more registered members than Chadema, the leading opposition party. So CCM doesn’t travel to campaign: it is organised in every street and village, working away from the media spotlight.

CCM is the party of the ground campaign network and that is why last year, at a supposed low-ebb of popularity, CCM won the local elections resoundingly – by 80% - against the same opposition coalition it is facing at the moment. The difference lay not in what was happening in the press or social media or rallies, but in how CCM managed its campaign.

7. The unexpected Magufuli

When John Magufuli, the respected but low profile Minister for Works entered the race for the CCM Presidential nomination, few commentators expected him to win. No international analysts included him in their likely list of victorious candidates. When he stood, there was no great courting of the media or mass tweets from support groups on the Internet. Indeed, his campaign was reminiscent of another unknown candidate in 1995 – Benjamin William Mkapa – who both won the nomination and then the General Election where he faced a former Deputy Prime Minister who had defected from CCM in an election many expected CCM to lose.


Mkapa – just like Magufuli today – was both unexpected, fresh, and the face of change – and because of this, difficult to define or attack. Twenty years later, facing a well-known former prime minister who defected from CCM, history appears to be repeating itself.

8. CCM’s superior delivery in rural Tanzania

I am a Member of Parliament for a rural constituency with a sizeable electorate. In 2010 – in another election believed to be tough for CCM to win – the party carried my constituency by over 80%, and nationwide by 61%. Recent professional opinion polling conducted across the country projects, in my constituency, a vote for CCM of nearly 90%. While there is much that is unique about my riding, there are many others that share common demographics.

The opposition is primarily a movement of the cities in a country that is predominantly agrarian and rural, and likes to portray countryside voters as uneducated and ignorant.  But whether people have a university degree, or access to the Internet, everywhere they vote on the basis of their interests. Across the world all voters when in the silence of the polling booth consider which party can best answer the question “What’s in it for me?” This is not a selfish choice, but the reality of what it means to be enfranchised in a pluralistic democracy.

CCM is answering that question. In 2000, only four villages in my constituency had electricity. Today, 44 do. This may not be the connectivity of rural Europe or America but the facts on the ground show that more children are in school, there more teachers and nurses more dispensaries, telecom services and paved roads than at any time in Tanzania’s history. Rhetoric that nothing has happened and therefore voters should replace CCM rings hollow in rural Tanzania where the majority of voters live.  And when CCM candidates say they will do more, on the basis of progress that they have witnessed, people believe them.

9. The stump speech: it’s about both the style and the substance

Elections are not just about promises but also about how those promises are packaged and delivered, and the stump speech by candidates is always telling. Lowassa has take to his platforms promising whatever he thinks his audience wants to hear. In one, he has gone so far to court votes in a particular region that he proposed to release Islamic fundamentalist terror suspects awaiting trial, accused of throwing acid in the faces of two British teenage aid workers.

While Lowassa’s speeches are short, Magufuli’s are detailed, outlining an agenda on education, jobs, healthcare, corruption, water services, and infrastructure. On polling day, voters remember how the candidate appeared and sounded when they addressed them. Did the voter hear the speech of a politician, or a president? On this score, Magufuli would appear to be winning.

10. The numbers

Tanzania does not have a culture of election polling, of focus groups, or campaigns based on voter research.  But we do have a long established culture of seeking public opinion on major policy decisions – from the change to multi-party politics to constitutional reviews. In 2005, election polling took place for the first time, predicting a landslide for CCM. And indeed CCM got 80% of the vote. In 2010, a poll by Ipsos-Synovate suggested that CCM’s share of the vote would fall to 61%. CCM disputed the polling results, believing that that it was too low. The final election outcome: CCM won 61% of the vote.

In this context, two polls have been published by reputable and independent organisations – Twaweza and Ipsos-Synovate - both using different methodologies, but with same outcome: CCM winning over 62% of the vote.

This election, the CCM has also engaged its own pollsters, running focus groups and a mass field survey of over 20,000 respondents up and down the country, across every region and demographic group. Some may believe that it is for politicians to make their case to the voters without first hearing their opinions: such people believe leaders should just get on and lead. We believe the best leaders are those who first listen. That’s what we have done, and our campaign has been based solely on what we know the voters want, and what CCM believes, in the real world, it can promise to deliver.

It is healthy to argue against the nine reasons for CCM’s victory. But analytical research – with a significant lead for CCM – is difficult to argue against. Yes, polls do swing. Polls can be imprecise. Polls can be wrong. But – typically – this is argument is made by the losing party, against the facts.

January Makamba

This publication was first appeared on Mail Guardian Africa  
read more

Sunday, October 18, 2015

Opinion: Edward Lowassa is not Tanzania’s Buhari

No comments

Tanzania may well need hang, but the incumbent party in the upcoming elections looks more likely to bring in that change than the opposition.

In debates about democracies in Africa, the victory of an opposition party in elections is often seen as a great indicator of progress. This makes sense up to a point in that it suggests a degree of political openness. But getting overly preoccupied with the idea of the incumbent losing can lead us to ignore the quality of leadership across competing parties.

On 25 October, the people of Tanzania will elect a new president, and as usual in elections, many candidates are presenting themselves as bold reformers and the harbingers of ‘change’. However, this election is not a referendum on whether the country needs change for the sake of change, but a referendum on “quality of leadership” and a choice between different potential presidents and their ability to lead. The new president will face major challenges both at home and abroad, where Tanzania’s role as a stabilising actor in Great Lakes region will be tested with the crisis in Burundi and a political transition in the DRC.

Simply put, Tanzanians are faced with two key questions. Which qualities of political leadership are most important for Tanzania to succeed? And which candidate has those qualities?

Inside the race to the presidency

The two main political parties in Tanzania’s presidential battle are the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) on the one hand, and the opposition CHADEMA – which is part of the opposition alliance Ukawa – on the other. Both of these parties have undergone some significant changes over the past few months, some for better, some for worse.

At the heart of these shifts has been each party’s choice of presidential candidate. During CCM’s nomination process, the ruling party knew that if it failed to make the right decision, it could be held captive by powerful factions, vested interests and influential foreign actors. Aware of the importance of the decision, CCM’s leadership used its veto power as a “custodian of national interest” in an attempt to rebalance the political playing field and end uncertainty caused by dangerous competing political factions. This process ended with the selection of Dr John Pombe Magufuli as its candidate.

Part of this selection saw former Prime Minister Edward Lowassa, who was linked to a struggle between reformists and vested interests within CCM, depart the ruling party. Lowassa had long been a party stalwart, but reformists were willing to upset some elements within the party if it meant they could get back into public’s good books regarding issues such as a corruption.

Lowassa’s history has been tainted by serious allegations. Firstly, he was relieved of his duties as a land minister under President Ali Mwinyi because of accusations of graft. And after he bounced back to become prime minister under President Jakaya Kikwete, he didn’t last long again as he was implicated in a high-level energy scandal. Lowassa is seen by many as an icon of corruption in Tanzania, and as a former US Ambassador put it in aleaked cable in 2008, “Lowassa’s corrupt activities have been an open secret throughout Tanzania for many years”.

On the other side of the political divide, CHADEMA had long portrayed itself as an alternative to CCM and in the past was credited for its ethical political stances and anti-corruption platform. However, the party under the broader Ukawa alliance had an eventful nomination process too, and in an unexpected twist of fate, arguably squandered its best opportunity to offer Tanzanians quality leadership when it decided to appoint Lowassa, who had by now defected from CCM, as its own presidential candidate.

Tanzania’s Buhari moment?

While political analysts stress how this could be Tanzania’s closest ever election, the reality is that a huge swing would be needed to unseat the ruling CCM. Two recent opinion pollsshow that some two-thirds of Tanzanians are planning to vote for CCM’s Magufuli. The opposition coalition led by CHADEMA has offered the electorate with old wine in new bottles. And by choosing Lowassa, the opposition has lost more than it has gained. Lowassa and Ukawa have had to drop an anti-corruption platform.

The election in Tanzania stands in stark contrast to Nigeria’s historic election in March in which the electorate was frustrated with President Goodluck Jonathan but saw his electoral rival Muhammadu Buhari as capable of solving the nation’s security crisis and of tackling corruption. Buhari’s campaign focused heavily on graft and, unlike Lowassa, he was able to make his case because he had a strong anti-corruption record. Similarly, when Mwai Kibaki ran as the candidate of a united opposition group in Kenya in 2002, he was only able to defeat ruling party candidate Uhuru Kenyatta with a campaign centred on anti-corruption because his reputation was relatively unsullied.

Unlike these victorious opposition candidates, Lowassa represents for many Tanzanians the very ills that the country wants to see addressed. This is evidenced by a group with vested interests still allegedly pouring money into his campaign with the assurance that these are investments will yield great fortunes. Moreover, Tanzanian national unity must be preserved as is an issue of national security and unfortunately Lowassa is seen to be adivisive figure with a ‘divide and rule’ mentality, locally  known as “stand up and be counted”.

Tanzania may well need change, but, perhaps paradoxically, it seems that voting for the incumbent CCM – Africa’s longest-ruling party – is more likely to usher in that change than the opposition.

Source: africanarguments.org

Author: Emmanuel Tayari - You can follow him on twitter at @mtanzania.

read more

Wednesday, September 16, 2015

Chama Cha Mapinduzi - TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

No comments

Tumewaita kuwaomba mtusaidie kufikisha ujumbe ufuatao kwa Watanzania:

Mwenendo wa Kampeni za CCM
Hadi jana, tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura. Kwa kuwa baadhi ya mikutano yetu inatangazwa moja kwa moja na redio za kijamii na luninga, wapiga kura waliopata nafasi ya kumsikia wanakadiriwa kufikia asilimia 70.

Tunafarijika na idadi kubwa ya watu wanaokuja kwenye mikutano ya kampeni zetu. Tunafarijika pia kwamba karibu Watanzania wote wanaopata fursa ya kumuona na kumsikia wamemuelewa na wamepata matumaini ya Tanzania Mpya kupitia kwake. Utafiti wetu wa ndani, tulioufanya kwa kipindi cha siku kumi zilizopita katika majimbo 246 kati ya majimbo 269, unaonyesha kwamba Dr. Magufuli atapata ushindi wa asilimia 69.3. Tunaamini kwamba asilimia hizi zitaongezek kadri Watanzania wengi zaidi wanavyopata fursa ya kumsikiliza Dr. Magufuli na kusikiliza
Ilani na sera za CCM.

Kwa upande wa kampeni zetu za Ubunge, zaidi ya robo tatu ya wagombea Ubunge wa CCM wamekwishazindua kampeni zao na wanaendelea vizuri. Sekretarieti ya Kampeni ya CCM inaanda program maalum ya kampeni katika majimbo yenye changamoto mahsusi. Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha wana-CCM kwamba viongozi na makada wengine wa CCM, waliopo madarakani na wastaafu watapita tena, jimbo kwa jimbo, nchi nzima katika siku 30 za mwisho katika jitihada za kuongeza ushindi wa CCM na Dr. Magufuli.

Midahalo ya Wagombea

Wiki tatu zilizopita, CCM, na kwa hakika vyama vingine pia, ilipokea mwaliko wa Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, kushiriki kwenye mdahalo wa wagombea Urais uliondaliwa na Baraza la Habari Tanzania (Media Council of Tanzania) kwa kushirikiana na taasisi nyingine kadhaa, ikiwemo Twaweza. Dr. Magufuli amekubali kushiriki katika mdahalo huo. Kwa msingi huo, kauli ya UKAWA iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Ndugu James Mbatia, kwamba UKAWA inaomba mdahalo ni njia ya kuwahadaa Watanzania tu kwa kuwa mwaliko wa mdahalo ulikwishatolewamapema kwa vyama vyote na wanaotakiwa kushiriki ni wagombea Urais wa vyama.

CCM inafurahishwa na utamaduni wa midahalo ambao unaanza kujitokeza katika chaguzi zetu. Na inaamini kwamba midahalo ya Wagombea Urais ni sehemu muhimu ya kuwashirikisha wapiga kura katika mchakato wa uchaguzi na kuwasaidia waamue nani wamchague kwa misingi ya hoja na sera na sio kwa ushabiki, kwa mihemko, na kwa propaganda. Mdahalo unatoa fursa ya wagombea kuulizwa maswali ya moja kwa moja na kutoa
ufafanuzi wa kina kuhusu sera na ahadi zao, fursa ambayo hawaipati kwenye mikutano ya hadhara kampeni.

Hatukubaliani na kauli ya UKAWA kwamba mdahalo usiwe baina ya wagombea bali uwe baina ya Wenyeviti wa Vyama. Tunaamini hoja hii ni kichekesho. Haijawahi kutokea popote duniani kwenye utamaduni wa midahalo, kwamba wagombea wasishiriki bali watu wengine ndio wafanye midahalo kwa niaba yao. Tunaamini mdahalo huu unapaswa kuwa baina ya wagombea. Wao ndio wanaoomba dhamana. Wao ndio wanaopaswa kujibu
maswali na kufafanua kuhusu ahadi zao. CCM inaamini kwamba ili mdahalo huu uwe na tija, wagombea Urais wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki. Mdahalo hautakuwa na maana
kama mgombea mmojawapo wa vyama vikuu atatengeneza kisingizio ili asishiriki.

UCHAGUZI WA AMANI

CCM inasikitishwa na kauli zinatolewa na baadhi ya viongozi wa UKAWA zenye kuashiria fujo na vurugu. Kauli kwamba kura zitaibiwa hazina msingi wowote. Kauli hizi zinaashiria maandalizi ya kushindwa na maandalizi ya kufanya vurugu baada ya matokeo ya kushindwa.

Utaratibu wa uchaguzi wetu unajulikana na umekubalika na vyama vyote. Kura zinapigwa kituoni na kuhesabiwa kituoni mbele ya mawakala wa vyama vyote, wasimamizi wa uchaguzi na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Baada ya kura kuhesabiwa, matokeo yanajazwa katika fomu ambayo kila wakala anasaini na kupewa nakala. Nakala ya matokeo hayo pia inabandikwa nje ya kituo cha kupiga kura. Kila Chama, na kila Mtanzania, kina fursa ya kujumlisha matokeo yake kwenye kila kituo na kupata jumla kuu. Matokeo ya nchi nzima yanajumlishwa mahala pamoja huku kukiwa na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi, pamoja
na wawakilishi wa vyama vyote na wao wakiwa na fomu zao za kila kituo nchi nzima.

Tunapenda kuwasihi Watanzania wasikubali vishawishi vya kufanya vurugu. Mara nyingi, viongozi wanaohamasisha vurugu wanakuwa na ulinzi au walinzi au uwezo wa kukimbilia pahala penye utulivu zaidi huku wakiwaacha wafuasi wao katika wakihangaika.

UCHAGUZI NA UMOJA WA KITAIFA

CCM pia inapenda kusisitiza imani yake kwamba uchaguzi haupaswi kutugawa kama taifa. Uchaguzi ni tukio la kupita. Kuna maisha baada ya uchaguzi. Kuna taifa baada ya uchaguzi. Lazima taifa liendelee kubaki moja, tuendelee kubaki wamoja. Tusitoe kauli za kupitiliza zenye mrengo wa kujenga chuki katika jamii na kuhatarisha umoja na amani ya nchi yetu.

Kama Chama kilichoasisi umoja wa taifa letu, tunaendelea kuasa kwamba wanasiasa wasijinadi kwa misingi ya udini, ukabila wala ukanda. CCM haina mpango kuendeleza mjadala wa kauli ya Mgombea wa UKAWA Ndugu Edward Lowassa aliyoitoa kanisani Tabora tarehe 6 September 2015 kwamba nchi ilishapata viongozi Wakatoliki na kwamba sasa ni zamu ya Walutheri kuchukua nafasi hiyo. Tunaamini mjadala huo hauna tija. Tunaamini kwamba Watanzania wengi, wa dini na madhehebu yote, hawaamini katika siasa za namna hii. Tuliamini kwamba UKAWA ingetumia
fursa ya mkutano wao na waandishi wa habari jana kuomba radhi kwa Watanzania. Kwakuwa hawakufanya hivyo, tunapendekeza mjadala wa jambo hili ufungwe. Itoshe tu kwamba Ndugu Lowassa amesema hivyo, Tume ya Uchaguzi imemuonya, na yeye hajajitokeza kuomba radhi wala kufafanua. Watanzania wamemjua ni kiongozi wa aina gani na watatoa hukumu yao tarehe 25 Oktoba 2015.

Imetolewa na
Ndugu Januari Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
16 Septemba 2015

read more

Msemo wa leo

No comments

" Mtu yoyote anaruhusiwa kusema chochote kuhusu lolote wakati wowote pahala popote bila hofu yoyote ili mradi havunji sheria yoyote."

~ January Makamba

read more