Showing posts with label Movies. Show all posts
Showing posts with label Movies. Show all posts
Wednesday, August 03, 2016
Tuesday, October 20, 2015
Trailer: Star Wars: The Force Awakens - Movie Trailer (Official)
Anglia Trailer ya Filamu ya Star Wars: The Force Awakens Trailer itakayoanzwa kuoneshwa December 8 Mwaka huu.
Upo tayari kwa Filamu hii??
Monday, October 12, 2015
Trailer: Hail, Caesar! - Movie trailer
Hail, Caesar ni movie yenye comedy,drama na music ambayo imetayarishwa kwa ustadi mkubwa, ikielezea maisha ya watengeneza filamu na mikasa wanayokutana nayo wakati wa utengenezaji wa filamu hizo. Mkasa mkubwa katika filamu hii ni pale Muigizaji mkuu wa filamu iliyokuwa inaandaliwa kutekwa.
Hail, Caesar! itaoneshwa kwa mara ya kwanza tarehe 5/2/ 2016. Starrings: Josh Brolin, George Clooney, Scarlett Johansson, Channing Tatum, Ralph Fiennes, Jonah Hill, Frances McDormand, Tilda Swinton, Dolph Lundgren, na wengine wengi.
Angalia Trailer yake hapa chini:
Friday, September 18, 2015
CHAPPiE: Filamu Kali Wiki hii.
Moja ya Filamu kali zilizotoka mwaka huu zinazohusu teknolojia ni nyingi ila chache kati ya hizo ni Blackhat, Furious 7 na CHAPPiE.
CHAPPiE ni Filamu iliyoigizwa nchini Afrika Kusini,Ambapo inaelezwa kwamba baada ya nchi hiyo kuchoshwa na vitendo mbalimbali vya uharifu katika jiji la Johannesburg, serikali yake inachukua uamuzi wa kununua teknolojia ya roboti wenye uwezo mkubwa wa kufikiri (Artificial Intelligence ) ili kulisaidia jeshi la polisi kukabiliana na matatizo hayo.
Lakini hapo badae mgunduzi (Dev patel) wa roboti hizo anataka kujribu mfumo mpya (Program) ambao utawanya roboti hao kuwa na hisia na makuzi kama ya binadamu lakini Bosi wake anamkatalia kujaribu mfumo huo.
Ndipo anapoiba roboti moja lililoaribika ilikujaribu huo mfumo, na hapo ndipo matatizo yanapoanza.
Filamu hii imechezwa na waigizaji maarufu kama Dev Patel ( ameigiza katika filamu ya Slumdog Millionaire ya 2008), Hugh Michael Jackman (Ameigiza filamu za X-men) na wengine wengi.
Itafute movie hii uitazame, NI KALI SANA.
Tuesday, September 08, 2015
Video: Jinsi Furious 7 (2015) ilivyotengenezwa. (Vitu Vingi ni Kweli)
Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa Filamu, hakika filamu ya Furious 7 itakuwa ni moja kati ya filamu ambazo hazichoshi kuangalia.
Wengi wamekuwa wakijiuliza Jinsi Filamu hiyo ilivyo tengenezwa, Ukweli ni kwamba vipande vingi vya Filamu hiyo vilichukuliwa katika mazingira ya ukweli.
Mfano ni kipande hiki ambacho Paul Walker’s Brian aliruka katika gari (Bus) liliokuwa linadondoka katika bonde kali.
Tazama Video hii kuona jinsi Furious 7 ilivyotengenezwa.
Je watengenezaji wa filamu Tanzania (Bongo movies) wanalipi lakujifunza kutoka kwa waandaaji wa Filamu za nje.
Subscribe to:
Posts (Atom)




