Utafiti mmoja uliofanywa nchini China umebaini kuwa ukila chakula kilichotiwa viungo kila siku unajiongezea maisha marefu.
Utafiti huo haswa umeonesha kuwa ukila chakula hususan pilipili utaishi maisha marefu zaidi duniani.
Watafiti mjini Baijing walidadisi maisha na vyakula wanavyokula wenyeji nusu milioni katika kipindi cha utafiti cha miaka 7.
Utafiti huo ulibaini kuwa wale waliokula chakula kilichojumuisha pilipili walikuwa katika hali bora zaidi kiafya wala hawakuwa katika hatari ya kuaga dunia.
Hali yao ya siha ilitofautiana sana ikilinganishwa na wale ambao waliweka viungo katika vyakula vyao chini ya siku moja kwa juma .
Watafiti hao walitoa tahadhari.
Wanasema kuwa utafiti huo ulikuwa wa ushahidi tu lakini wakashauri utafiti zaidi ufanyika kwengineko ilikutilia pondo utafiti wao.
Hata hivyo walibaini kwa uhakika kuwa kiungo kinachopatikana katika pilipili, 'capsaicin' kinauwezo wa kupigana na seli zinazotuma ujumbe kwa ubongo kuwa mtu amezeeka na kusababisha viashiria vya utu uzima.
CHANZO: BBC Swahili