Baada ya kuwepo kwa uvumi wa kipindi kirefu kuwa kampuni ya apple inampango wa kutengeneza magari yake hatimaye siri zimeanza kuvuja.
Kulingana na ripoto iliyochapishwa katika tovuti ya The Wall Street Journal, vyanzo vya kuaminika kutoka kampuni hiyo inayofanya vizuri katika vifaa vya teknolojia za mawasilianio na electronics, vimesema kuwa kampuni hiyo itaanza kuuza magari yake yanayotumia nishati ya umeme ifikapo mwaka 2019.
Licha ya kuwepo na kampuni nyingine nyingi kama Tesla ambazo tayari zinatengeneza magari yanayotumia nishati ya umeme, badi apple imedhamiria kujiingiza katika biashara hiyo.
Je, wataleta mapinduzi yoyote kama yale waliyo fanya katika computer na simu za kiganjani?