Utawala wa kifalme nchini Swaziland unaongozwa na mfalme Mswati umetakiwa kufutilia mbali sherehe maarufu za kitamaduni baada ya wasichana kadha waliokuwa wakisafiri kwenda kwa sherehe hizo kufa kwenye ajali ya barabarani.
Kundi linalounga mkono demokrasia nchini humo la (the Swaziland Solidarity Network) limetoa wito kwa mfalme Mswati kufutilia mbali sherehe hizo ambazo wasicha walio nusu uchi hucheza mbele ya mfalme.
Kundi hilo linasema kuwa zaidi ya wasichana 60 waliangamia wakati lori walilokuwa wakisafiria lilihusika kwenye ajali ya barabarani.
Utawala nchini Swaziland unasema kuwa idadi ya wasichana waliokufa ni 13.