Thursday, August 13, 2015

#whatWEsay: UKIWA MUONGO USIWE MSAHAULIFU SIKIA HII

No comments

Muongo alikuwa akiwahadithia watu jinsi alivyokuwa akipambana na rushwa na ufisadi nchini mwake. Mara simu yake ikaita, ....akakatisha hadithi yake sehemu alipomkamata fisadi mmoja papa. 
Baada ya kumaliza kuongea na simu akauliza niliishia wapi kuhadithia? Wakamjibu kumkamata fisadi mmoja papa. Akaendelea....." Aaaah basi nikamfanyisha sala ya toba na muda mchache tu baada ya ile sala ya toba nikagundua yule bwana ni msafi kweli, hana doa, ni mpiganaji na mtetezi wa wanyonge, alipokuwa anaiba hakujua kwa nini alikuwa anaiba....

Watu wakajiuliza kimoyo moyo....Huyo huyo fisadi papa? wakaguna Mh!! Muongo hakujali akaendelea kuwa bize na story.....Basi nikaanza kushirikiana nae katika vita yetu ya kupambana na ufisadi. 
Tuliwakemea wote walotaka kuwa madalali wa gesi na mafuta, hatukupokea hongo ila tuliwasaidia vijana vijisenti vidogo vya kuandamana nasi katika mapambano. Watu wakasema acha hizoooo, we mjinga nini, tokea lini fisadi papa akaonesha uzalendo kama huu?

#whatWEsay ni mfululizo wa habari zinazoelezea jinsi gani wananchi wanautazama uchaguzi ujao.

HAYA SIO MAONI YA CNT