Friday, September 18, 2015
CHAPPiE: Filamu Kali Wiki hii.
Moja ya Filamu kali zilizotoka mwaka huu zinazohusu teknolojia ni nyingi ila chache kati ya hizo ni Blackhat, Furious 7 na CHAPPiE.
CHAPPiE ni Filamu iliyoigizwa nchini Afrika Kusini,Ambapo inaelezwa kwamba baada ya nchi hiyo kuchoshwa na vitendo mbalimbali vya uharifu katika jiji la Johannesburg, serikali yake inachukua uamuzi wa kununua teknolojia ya roboti wenye uwezo mkubwa wa kufikiri (Artificial Intelligence ) ili kulisaidia jeshi la polisi kukabiliana na matatizo hayo.
Lakini hapo badae mgunduzi (Dev patel) wa roboti hizo anataka kujribu mfumo mpya (Program) ambao utawanya roboti hao kuwa na hisia na makuzi kama ya binadamu lakini Bosi wake anamkatalia kujaribu mfumo huo.
Ndipo anapoiba roboti moja lililoaribika ilikujaribu huo mfumo, na hapo ndipo matatizo yanapoanza.
Filamu hii imechezwa na waigizaji maarufu kama Dev Patel ( ameigiza katika filamu ya Slumdog Millionaire ya 2008), Hugh Michael Jackman (Ameigiza filamu za X-men) na wengine wengi.
Itafute movie hii uitazame, NI KALI SANA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)