Friday, May 29, 2015
Biashara ya namba za simu Tanzania yawa kero.
Kumekuwa na malalamiko mengi kuwa mitandao ya simu Tanzania imekuwa ikiuza laini za simu ambazo namba zake zimekwisha tumika na mtu mwingine na kisha kusumbuliwa na watu waliotumia namba hiyo.
Mwezi huu mwanzoni nilinunua laini ya mtandao wa vodacom, mara tuu nilipoanza kutumia laini hiyo nikapigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mmiliki wa namba hiyo na kunitaka ni mrudishie, na alikuwa tayari kulipa kiwango flani cha pesa ili aipate laini hiyo.
Maswali niliyojiuliza:-
1. je serikali imeruhusu jambo hili?
2. Kama ndiyo, waliweza fikiria matatizo yanayoweza tokea baada ya mtu kuuziwa laini hiyo?
Mfano: kama namba hiyo ilitumika kufanya uharifu na mtumiaji huyo hakukamatwa, kisha akauziwa mtu mwingine, huko si ni kuuziana kesi jaman?
3. Je, Mitandao ya simu ilikubaliana na wenye namba hizo kufanya biashara hiyo. Maana hawawezi kujua kwanini mtumiaji alishindwa ku renew namba hyo kwa wakati.
4. Je, watumiaji wapya wa namba hizo wakikutwa na janga lolote, mitandao hiyo ipo tayari kulipa fidia.
Ni vyema kutafuta njia nyingine ya kuweza kutengeneza namba mpya za simu kiliko hii ya kuuza namba za simu zilizotumika na watu wengine, kwani hatujui ni kwa sababu ipi ilizifanya zisitumike. Kama na wewe umekutwa na janga hili usisite kutujulisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)