Monday, September 14, 2015

Misri yaomba radhi

No comments

Misri imeomba radhi baada ya watu 12, wakiwemo watalii raia wa Mexico kuuawa kwa bahati mbaya na vikosi vya usalama wakati wa Operesheni dhidi ya ugaidi.

Wizara ya mambo ya ndani ya Misri imedai kuwa kundi hilo la watu liliingia kwenye eneo lililopigwa marufuku.

Nchi hiyo imekuwa ikipambana na wanamgambo wa kiislamu kwa miaka kadhaa huku mashambulizi yakishika kasi tangu kuondolewa madarakani kwa Rais Mohammed Morsi mwaka 2013.

Mbali na kuwa jangwa la magharibi ni kivutio cha utalii, limekuwa la hatari kwasababu ya kuzorota kwa usalama nchini Libya.

Raia kumi wa Mexico na wa Misri walijeruhiwa katika operesheni hiyo.Maafisa usalama wamesema idadi ya watalii wa Mexico waliouawa ni wanane na wamisri wanne ingawa idadi hiyo ya Raia wa Mexico haijathibitishwa na Mexico yenyewe.

Waziri Mkuu wa Misri,Ibrahim Mahlab ameomba radhi kwa njia ya simu alipozungumza na Balozi wa Mexico jijini Cairo,Al-Yawm al-Sabi.Tovuti ya nchi hiyo ilimnukuu.

Chanzo:BBC Swahili