Thursday, September 10, 2015

Walemavu wa macho kupiga kura wenyewe

No comments


Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, watu wenye ulemavu wa macho watashiriki katika kumchagua kiongozi wanayemtaka kwa kutumia kifaa maalum chenye maandishi ya nukta nundu au Braille katika uchaguzi mkuu utakofanyika Oktoba 25 waka huu.

Vifaa hivyo vitaanza kufanyiwa majaribio mwishoni mwa mwezi huu ambapo watu hao wataweza kufundishwa jinsi ya kupiga kura bila ya kuwa na mtu wa kumsaidia au kumwongoza kupiga.

Kumekuwa na madai kuwa wale waliokuwa wakiwasaidia watu wenye ulemavu wa kuona mara nyingi huwapotosha walemavu hao kwa kupiga kura kinyume ya matarajio ya mlemavu huyo.

Tangu jadi walemavu wa macho wamekuwa wakishiriki katika kupiga kura kwa kusaidiwa na watu ambao huwa wanenda nao katika vituo vya wa kupigia kura kwa lengo la kuwaelekeza wakati mwingine husaidiwa na mawakala au wasimamizi wa vituo vya kupigia kura.

Chanzo: BBC